BBC imefahamu kuwa chama cha riadha cha kenya kumepata ripoti inayoonyesha kuwa wanariadha wawili wa Kenya wa mbio za masafa marefu, ambao bado hawajatajwa wamepatikana na hatia ya kutumia dawa za kuongeza nguvu za mwili.
Chama hicho kinachelewa kutaja majina ya wanariadha hao kuzuia kuharibu sherehe za kumkaribisha mwanariadha Mary Keitany ambaye alishinda mbio za London Marathon wiki iliyopita na kuvunja rekodi ya dunia.
- Mkenya mshindi wa Olimpiki abainika kutumia dawa za kusisimua misuli
- Mke na mumewe kutoka Kenya washinda mbio za Paris Marathon
- Wakenya watawala mbio za London Marathon
- Mkenya ashinda Marathon New York
Wiki tatu zilizpita mwanariadha mwingine mkenya na mshindi wa zamani wa mbio za London Marathon Jemima Sumgong, alipigwa marufuku kwa kupatikana kutumia dawa za kuongeza nguvu za mwili.
Baadhi ya wanariadha maarufu wa Kenya wana hofu kuwa sakata hizo huenda zikachafua mafanikio yao na wametaka hatua kali kuchukuliwa dhidi ya wahusika.
Post a Comment