Rais wa zamani wa Zambia Kenneth Kaunda, mmoja wa viongozi wa mwisho walio hai barani Afrika walioshiriki katika kupigania uhuru wa nchi zao ametimiza miaka 93.
Bwana Kaunda aliongoza Zambia kupata uhuru mwaka 1964 na kuwa rais wake wa kwanza.
Baadhi ya raia wa Zambia wamekuwa wakisambaza picha ya baba mwanzilishi wa taifa hilo.
Picha iliyo china hapa ni kutoka kwa kumbukumbu wakati bwana Kaunda alikuwa akishiriki kwenye mazungumzo na waingereza mwaka 1961.
Post a Comment