0
Korea kaskazini inaluamiwa kwa kuonyesha silaha bandia katika maonyesho ya hivi majuzi ya ubabe wake wa kijeshi.
Afisa wa zamani wa masuala ya ujasusi anasemna baadhi ya bunduki na makombora yaliyotumiwa kwenye maonyesho hayo yalikuw bandia.
Michael Pregent alikiambia kituo cha runinga cha Fox kuwa baadhi ya bunduki zilizokuwa kwenye maonyesho hayo zilikuwa ni za kujekesha
Lakini maonyesho kama hayo kuonyesha ubabe wa kijeshi yametumiwa kwa miongo kadha.
Maonyesho ya kijeshi mjini PyongyangHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMaonyesho ya kijeshi mjini Pyongyang
Kwa sasa msukosuko ni mkubwa kati ya Marekani na Korea Kaskazini.
Hii ni baada ya rais wa Marekani kuapa kuwa ni lazima atakabiliana na tisho la Korea Kaskazini.
"Sio kuwa Korea kaskazini inafikiri kuwa itashinda Marekani lakini kile itafanya ikiwa itashambuliwa," bwa Pregent alisema.
Wanajeshi wa Korea KaskaziniHaki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionWanajeshi wa Korea Kaskazini

Historia ya silaha bandia

Vifaru bandia vilitumiwa na Uingereza wakati wa vita vya pili vya dunia kuonyesha ubabe wa kijeshiHaki miliki ya pichaNATIONAL ARCHIVES
Image captionVifaru bandia vilitumiwa na Uingereza wakati wa vita vya pili vya dunia kuonyesha ubabe wa kijeshi
Silaha hizi bandia zilitengenezwa kukwepa mashambulizi ya angani na kuwachanganya marubani ya jeshi kushambulia vifaru bandia baada ya vifaru halali
Wasani ya jeshi la Ufaransa nao walichora mito bandia na mitaro ili kuwachanganya marubani wa ndege za vita.
Ujanja kama huo pia ulitumiwa wakati wa vita vya pili vya Dunia
Vifaru bandiaHaki miliki ya pichaNATIONAL ARCHIVES
Image captionVifaru bandia
Mruka na mwavuli bandia wakati wa vita vya pili vya duniaHaki miliki ya pichaNATIONAL ARCHIVES
Image captionMruka na mwavuli bandia wakati wa vita vya pili vya dunia

Miongo kadha kabla miti ilitumika kupigana katika vita vya wenyewe nchini Marekani

Miti hii ilipakwa rangi hadi kifanana na silaha ya kurusha makombora.
Lengo lilikuwa ni kuwachanganya maadui kuhusu ni wapi kulikuwa na adui.
Bunduki bandia za mitiHaki miliki ya pichaCORBIS/GETTY IMAGES
Image captionBunduki bandia za miti
Aina hii ya silaha bandia zilitumika karne za 18 na 19
Picha hii inaonyesha wanajeshi wa Ujerumani wakikimbia ndani ya vifaru bandia miaka ya 1920
Wanajeshi wa Ujerumani wakikimbia ndani ya vifaru bandiaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES/HULTON ARCHIVE
Image captionWanajeshi wa Ujerumani wakikimbia ndani ya vifaru bandia

Post a Comment

 
Top