Rais Magufuli wa Tanzania amewafuta kazi wafanyikazi 10,000 wa serikali kwa kuwa na vyeti bandia vya elimu.
Amewaagiza kuwacha kazi ifikiapo Mey 15 la sivyo wakamatwe na kushtakiwa.
Hatua hiyo inajiri baa wafanyikazi hao kupatikana na vyeti bandia vya shule.
Kulingana na ripoti iliopokewa na rais Magufuli, takriban wafanyikazi 10,000 wa serikali wana vyeti ghushi vya shule.
Maelezo hayo yaliotolewa katika mji mkuu wa Dodoma yanaonyesha wafanyikazi 9,932 wa serikali walipatikana na vyeti bandia vya shule ya upili
Mwandishi wa BBC Sammy Awami anasema kuwa hiyo ni asilimia 2 ya wafanyikazi wote wa serikali wapatao 435,000.
- Magufuli: Hamuhitaji cheti cha kuzaliwa kufunga ndoa
- Waziri aagiza Nay wa Mitego aachiliwe huru Tanzania
- Jaji mkuu atimuliwa kwa kutotoa vyeti vya ndoa za jinsia moja
Akizungumza baada ya kupata ripoti hiyo, rais Magufuli amewapatia maafisa walio na vyeti hivyo wiki chache za kujiuzulu la sivyo washitakiwe.
Pia ameyataka magazeti nchini humo kuchapisha majina ya maafisa hao.
Post a Comment