Mwanariadha wa mbio za masafa marefu kutoka nchini Kenya, Jemima Sumgong aliyeshinda medali ya dhahabu katika mashindano ya mbio za marathoni olimpiki mjini Rio mwaka jana pamoja na mashindano ya mbio za london marathoni ,amebainika kuwa ni miongoni mwa watu wanaotumia dawa za kusisimua misuli .
Shirikisho la riadha duniani,IAAF limesema kuwa majibu waliopata kutoka katika uchunguzi wa kina katika damu ya mwaariadha huyo umeonyesha kuwa anatumia dawa za kusisimua misuli ambazo zinamsaidia kukimbia kwa nguvu na kwa muda mrefu.
Mpaka sasa hakuna tamko lolote lililotolewa kutoka kwa mamlaka husika juu ya adhabu itakayotolewa baada ya majibu ya matokeo ya vipimo vya mwanariadha huyo.
Post a Comment