Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema Sergio Aguero alitumia werevu baada ya kugongwa kwa kichwa na Marouane Fellaini.
Fellaini, 29, alioneshwa kadi nyekundu moja kwa moja dakika ya 84, sekunde chache baada yake kuoneshwa kadi nyingine ya manjano kwa kumtega nyota huyo wa Argentina.
Mechi hiyo ya Ligi ya Premia ilimalizika sare tasa.
"Sikutazama tukio hilo lakini naweza kufikiria kwamba labda kadi nyekundu na ilitokana na uchezaji wa uzoefu, na ujanja kiasi wa mchezaji huyo wa Argentinia," alisema Mourinho.
Alipoulizwa iwapo kiungo wa Ubelgiji Fellaini hakutumia busara, Mourinho alisema: "Marouane anasema ilikuwa kadi nyekundu kwa sababu yeye ni Marouane.
"[Mwamuzi] Martin Atkinson aliniambia kwa maoni yake ilikuwa kadi nyekundu, lakini nilimuona Aguero baadaye na hakuwa ameumia pua, hakuwa na jeraha kichwani, na uso wake ulikuwa na tabasamu kama kawaida. Sina uhakika…
"Iwapo Sergio hangejiangusha basi bila shaka haingekuwa kadi nyekundu, lakini Marouane alimpa fursa ya kufanya hivyo ….Sijui, lakini ninachokifahamu ni kwamba tulicheza dakika 15 na wachezaji 10 na vijana wetu walicheza vizuri sana, walipigania kuondoka na alama moja."
Felliani sasa amefukuzwa uwanjani mara tatu tangu ajiunge na United kutoka Everton kwa £27.5m mwezi Septemba 2013.
Awali, alifukuzwa uwanjani wakati wa mechi iliyomalizika sare tasa na Hull City mnamo 24 Mei 2015 na mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Real Sociedad mwezi Novemba 2013.
Fellaini pia alifukuzwa wakicheza mechi iliyomalizika sare 1-1 akichezea Everton dhidi ya Bolton katika Ligi ya Premia 2010.
Post a Comment