0
Misri imeweka rekodi kwa kufanikiwa kufuzu kwa mara ya tisa katika fainali za kombe la Afrika baada ya kuishinda Burkina Faso 4-3 katika mikwaju ya penalti baada ya sare ya 1-1.
Mlinda lango wa miaka mingi Essam El Hadary alithibitisha ushujaa wake kwa kuokoa penalti iliopigwa na Betrand Traore ili kupata ushindi huo.
Wakati wa muda wa kawaida Mohamed Salah aliiweka kifua mbele Misri baada ya kufunga bao zuri.
Hatahivyo Burkina Faso walisawazisha wakati Aristide Bance alipofunga krosi iliopigwa na Charles Kabore.
Kupitia bao hilo Burkina Fasso imekuwa timu ya kwanza kuifunga Misri katika mchuano huo.
Wachezaji wa Burkinabe ambao ndio walioonyesha mchezo mzuri wakati wa muda wa kawaida walianza penalti hizo kwa kufunga, lakini Misri ikaibuka mshindi baada ya Traore kushindwa kucheka na wavu.

Post a Comment

 
Top