Mahakama ya haki ya kimataifa ya Hague ICJ imeipendelea Somalia katika kesi ya mpaka kati yake na Kenya.
Somalia inataka mpaka kuongezwa keulekea eneo la Kusini lakini kenya inadai kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kuingilia kati.
Nchi hizo mbili zimekuwa kwenye mzozo kwa miaka mingi kuhusu sehemu ya bahari ya Hindi, ambayo inaaminiwa kuwa na utajiri wa mafuta na gesi.
Mahakama huyo ilikataa ombi la kenya kuwa makubaliano yaliyoko kati ya nchi hizo, yanatosha kupatikana kwa suluhu ya mzozo huo wa mpaka.
Uamuzi huo unamaanisha kuwa kesi hiyo ya mpaka iliyowasilishwa mahakamani na Somalia itaendelea.
Post a Comment