Waziri wa mambo ya nje wa Iran Javad Zarif ameitaka Marekani kukoma kutoa witisho kwa taifa hilo.
Kwenye mahojiano na BBC, Bw Zarif ameituhumu serikali mpya ya Rais Donald Trump kwa kujaribu kuchochea na kuichokoza Iran kwa kuandaa vikwazo vipya dhidi ya taifa hilo.
Hii ni baada ya Iran kufanyia majaribio kombora la masafa marefu hivi majuzi.
Bw Zarif ametahadharisha kuwa iwapo vikwazo zaidi vitawekewa Tehran, badi nchi hiyo ina hatua za kulipiza kisasi ambazo nayo inaweza kuzichukua.
Alikuwa akiongea pambizoni mwa mkutano mkuu kuhusu usalama ambao unafanyika mjini Munich, Ujerumani.
Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence, katika mkutano huo, alidai Iran ndiyo mfadhili mkuu wa ugaidi.
Post a Comment