0
Tanzania inasema kuwa itapokea dola milioni 305 kama mkopo kutoka kwa Benki ya Dunia, kugharamia upanuzi wa bandari kwenye mji wa Dar es Salaam.
Bandari hiyo ndiyo inaunganisha mataifa ya Afrika ambayo hayapakani na bahari yakiwemo Zambia, Rwanda, Malawi, Burundi na Uganda na pia eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.
Benki ya Dunia ilisema katika ripoti ya mwaka 2014 kwa matatizo kwenye bandari ya Dar es Salaam yalikuwa yakiigharimu Tanzania na majirani zake hadi dola milioni 2.6 kila mwaka.

Post a Comment

 
Top