0
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amesema ana wasiwasi mkubwa kwamba karibu thuluthi mbili ya majimbo 36 nchini humo hayana uwezo wa kuwalipa waanyakazi mishahara, licha ya kupokea udhamini kutoka kwa serikali ya shirikisho.
Rais Buhari amesema atajaribu kuwasilisha fedha zaidi lakini ameonya kwamba serikali kuu pia inakabiliwa na mataizo ya fedha.
Ni hivi maajuzi tu ambapo maafisa katika jimbo lililopo kaskazini mashariki mwa nchini hiyo, waligundua uhuni wa kuwalipa mishahara wafanyakazi hewa wa serikali.
Hatua zilichukuliwa kuwasaka na kuwaondosha wafanyakazi hao hewa kutoka orodha ya wafanyakazi wa serikali, na mamilioni ya dola yaliokolewa.
Nigeria, ambayo ni nchi inayozalisha mafuta ya kiwango kikubwa Afrika, imeathirika pakubwa na kushuka kwa bei za mafuta.

Post a Comment

 
Top