0

Rais wa Marekani Donald Trump amemfuta kazi kaimu mwanasheria mkuu Sally Yates saa chache tu baada ya kuwaagiza mawakili wa idara ya haki nchini humo kutotetea uamuzi wa kuwawekea vikwazo raia wanaotoka katika baadhi ya mataifa ya kiislamu.
Taarifa ya Ikulu ya Whitehouse imemshtumu kwa usaliti.
Sally Yates ambaye aliteuliwa na Obama alisema kuwa hafikirii kwamba marufuku hiyo ya muda kwa raia wa mataifa saba ya Kiislamu ni halali.
Wadhfa wake umechukuliwa na kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya kijimbo huko Virginia Dana Boente.
Agizo hilo la rais lililotiwa saini Ijumaa iliopita limesababisha maandamano nchini Marekani na ughaibuni.
Awali kundi moja la wanadiplomasia liliandika barua likikosoa agizo hilo wakisema litazidi kuhatarisha usalama wa taifa hilo.
Taarifa hiyo ya ikulu imesema kuwa bi Yates ni dhaifu kuhusu mipaka na dhaifu zaidi katika maswala ya uhamiaji
Hatahivyo wanachama wa Democrat walipuuzilia mbali kufutwa kwake.
Seneta Chuck Schumer ,kiongozi wa chama alisema katika taarifa kwamba mwanasheria mkuu anafaa kuwa mtiifu kwa sheria na sio ikulu ya Whitehouse.

Post a Comment

 
Top