0
PHONE NO:+255624031936 or +255768550136
TOVUTI:sitenewztanzania,blogspot,com
Na Magdalena Marko
Hujambo na karibu mpeenzi msomaji katika mfululizo wa makala ya AFYA YA JAMII ambapo kwa siku ya leo tutaangalia tunda aina ya nanasi.twende pamoja.
Nanasi ni tunda la kitropiki, linapendwa na walaji wengi kwa sababu ya ladha yake tamu na harufu yake nzuri. Tunda hili laweza liwa mara tu baada ya kuvunwa, baada ya kulipika, au kama juisi. Nanasi ni chanzo kizuri cha vitamin A na B, pia inakiwango kingi tu cha vitamin C pamoja na madini kama vile: patasiam, magnesiam, kalsiam, na madini chuma.
Asili ya nanasi inaaminika kuwa ni Brazil na Paraguay huko Amerika ya Kusini. Hapa Tanzania, nanasi hulimwa zaidi maeneo ya Bagamoyo, Kibaha (Pwani), Tanga, Mtwara, Lindi, Geita na Mwanza. Lakini pia maeneo yote ya pwani ya Tanzania yanafaa kwa kilimo cha nanasi.Mananasi ni matunda ambayo yanalimwa katika ukanda wa joto.
uchunguzi unaonyesha mananasi Hayahitaji maji/mvua nyingi ili kustawi ila yanahitaji kupaliliwa ili kuondoa magugu. Vilevile, yanastawi zaidi pale ambapo yanapandwa katika udongo unaopitisha maji kwa urahisi. Ni zao ambalo ni rahisi sana kulima lakini linahitaji maandalizi pamoja na uvumilivu wa kutosha hadi kutoa matunda.
Tunasema ni rahisi kwa sababu halihitaji virutubishi kama yalivyo mazao mengine (mfano: mahindi, mpunga) na vile vile halihitaji madawa kwa ajili ya kutunza zao lako. Uvumilivu unahitajika kwani nanasi huchukua wastani wa miezi 18 hadi 24 (mwaka mmoja na nusu hadi miwili) toka kupanda hadi kuvuna.
Kwa kawaida, hapa Tanzania maandalizi ya kupanda mananasi huanza kufanywa mwanzo wa kipindi cha mvua za vuli. Tathmini fupi ya mahitaji (requirements)
kulingana na uzoefu wa kilimo-maarifa ni kama ifuatavyo. Tathmini hii imefanyika kwa kuzingatia ukubwa wa shamba lenye ukubwa wa acre moja
KiIimo cha nanasi kinapendelea hali ya hewa ya joto na husitawi vema katika mwinuko kati ya mita 0-1750 kutoka usawa wa bahari. Mwinuko wa mita 1300 hadi 1750 hufaa zaidi kwa uzalishaji wa nanasi kwaajili ya kusindika na mwinuko chini ya hapo hufaa zaidi kwaajili ya ulaji wa moja kwa moja. Mahitaji ya joto ni kati ya nyuzi joto 18°C hadi 35°C
Kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho hadi wakati mwingine kwaheri kwa sasa.

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top