0
Mwenyekiti mpya wa Muungano wa Afrika AU rais wa Guinea Alpha Conde, amewalaumu vikali marais ambao hufika mikutano wakiwa wamechelewa au hutoka mapema.
Akitoa hotuba wakati wa kufamalizika kwa mkutano wa kila mwaka wa AU nchini Ethiopia bwana Conde alisema:
"Kuanzia sasa tutaanza kwa wakati. Kama tunasema ni saa nne kamili ni lazima tuanze saa nne kamili. Tunawezaje kusema kuwa wakati tuna mikutano na nchi za nje tunafika kwa wakati hata kama ni China,Japan au India? Mbona hatuwezi kufika kwa wakati mikutano yetu?"
Shirika la AFP linasema kuwa matamshi ya Conde yaliungwa mkono kwa wingi na waakilishi wa chini kwa kuwa viongozi wengine walikuwa tayari wametoka ndani ya ukumbi huo wa AU.
Conde pia alilamikia kushindwa kwa AU kuboresha mifumo yake ya kiteknolojia.
"Unawezaje kusema kuwa mtandao kwenye makao yetu ni mbaya wakati majirani wetu ambao ni tume ya masuala ya uchumi ya Umoja wa Mataifa, mtandao wao uko shwari?
Bwana Conde alichukua wadhifa huo wa mwenyekiti unaozunguka kutoka kwa rais wa Chad Idriss Deby.

Post a Comment

 
Top