0
Mgombea urais wa chama kikuu cha upinzani nchini Zambia ameishutumu tume ya uchaguzi kwa kupanga na chama tawala kumuibia kura siku ya alhamisi.
Chama cha Hakainde Hichilema kimejiondoa katika mchakato wa kuhakiki kura baada ya kulalamika kuwa kuna kiasi kikubwa cha udanganyifu, huku akitoa mfano wa kukiukwa kwa taratibu.
Wakati mchakato wa kuhesabu kura ukiendelea, Rais aliye madarakani Edgar Lungu, anaongoza kwa tofauti chache ya kura dhidi ya mpinzani wake wa karibu bwana Hichilema.
Hakainde Hichilema ambae ni mara yake ya tano kugombea urais anadai kuwepo kwa udanganyifu katika upigaji kura siku ya alhamisi.
Chama chake kinataka kura zihesabiwe tena upya kakika mji mkuu Lusaka baada ya kuonesha ukiukwaji wa taratibu.
Rais aliye madarakani Edgar Lungu, anaendelea kuongoza kwa zaidi ya nusu ya kura ambazo zimehesabiwa hadi sasa.
Wakati huo huo rais Lungu ametoa wito kwa wazambia wote kuwa watulivu na kuheshimu matakwa ya watu

Post a Comment

 
Top