Mpatanishi mkuu wa muungano wa upinzani nchini Syria amejiuzulu katika kile anachosema kuwa, kuvunjika kwa mazungumzo ya amani, yenye nia ya kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu miaka mitano sasa.
Mohammad Alloush, anayetoka kwenye kamati kuu ya upatanishi HNC, amesema kuwa anajiondoa kwa sababu mazungumzo hayo yanayoungwa mkono na Umoja wa mataifa huko Geneva, hayajazaa matunda au kutanzua matatizo wanayopitia raia wa Syria waliozingirwa na vita.
Kamati kuu ya mazungumzo hayo ya amani iliahirisha shughuli zake mwezi Aprili na hakuna tarehe ambayo imewekwa ya kurejelewa kwa mazungumzo.
Post a Comment