0
Waziri wa maswala ya kigeni wa Uturuki ameushtumu Muungano wa Ulaya kwamba unaidhalilisha nchi yake.
Akizungumza na gazeti la Ujerumani , Bild, Mevlut Cavusoglu amesema badala ya kuisaidia Uturuki baada ya jaribio la mapinduzi, muungano huo umekuwa ukiitishia kwa kuitukana.
Mataifa ya muungano huo yanasema kuwa msako ulioidhinishwa na rais wa Uturuki , Recep Tayyip Erdogan, huenda ukakiuka masharti ambayo ni lazima taifa hilo iafikie, kabla ya kufuzu kupata cheti cha usafiri huru katika mataifa ya muungano huo, na pia majadiliano ya kuwa mwanachama wa muungano huo.
Zaidi ya watu 23,000 wamekamatwa huku wengine 10,000 wakisimamishwa kazi ama hata kufutwa .wanatuhumiwa kwa kuiunga mkono kiongozi wa mapinduzi Fethulah Gullen .hatahivyo kiongozi huyo wa dini amekanusha kutekeleza kitendo chochote kama hicho.

Post a Comment

 
Top