Zaidi ya watu 125 wamefariki katika mashambulizi mawili ya bomu yaliyokumba mji mkuu wa Iraq Baghdad.
Watu wengine 130 wamejeruhiwa vibaya katika mashambulizi hayo yaliyodaiwa kutekelezwa na kundi la wanamgambo wa kiislamu la Islamic State.
Kundi la Islamic State lilidai kuhusika kwenye shambulizi hilo ambapo bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari lililipuka karibu na mkahawa katika wilaya ya Karada na kuwaua takriban watu 6.
Zaidi ya watu 20 na walijeruhiwa.
Bomu la pili lililipuka baadaye kaskazini mwa mji wa Baghdad.
Milipuko hiyo inatokea wiki moja baada ya wanajeshi wa Iraq kuukomboa mji wa Fallujah kutoka kwa Islamic State.
Post a Comment