0
Kamati ya maadili ya FIFA imependekeza kifungo cha walau miaka sita kwa aliyekuwa Rais wa shirikisho la soka la Afrika kusini, Kirsten Nematandani kwa madai ya kuhusika kwenye vurugu katika mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyofanyika Afrika kusini mwaka 2010.
Miaka minne iliyopita alisimamishwa baada ya FIFA kupata ushaidi kuwa mechi ilipangwa na wabashiri washirika kutoka mashariki ya mbali.
Sambamba na hilo wachunguzi wa FIFA wamesema wamependekeza kifungo kirefu kwa aliyekuwa Rais wa wajumbe wa shirikisho la mpira wa Miguu la Zimbabwe, Jonathan Musavengana na kocha wa zamani wa Togo, Banna Tchanile, kwa madai ya kupokea hongo na rushwa.
Matokeo ya uchunguzi yatapitishwa kwenye jopo la majaji wa FIFA ili kufanya maamuzi.

Post a Comment

 
Top