0
Winga wa Manchester United Adnan Januzaj, amejiunga na sunderland kwa mkopo msimu huu wa 2016/17.
Uhamisho huo umemuunganisha na meneja wake wa zamani David Moyes pamoja na wachezaji weza Donald Love na Paddy McNair aliyejiunga na timu hiyo kwa kitita cha pauni milioni 5.5 wiki hii.
Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Ubeligiji, Januzaj, alikuwa anataka kutoka Old Trafford kabisa lakini klabu hiyo ya United iliamua kumkabidhi kwa klabu hiyo kwa mkopo.
Adnan Januzaj (kulia)
Image captionAdnan Januzaj (kulia)
Januzaj alifunga mabao matano katika mechi 63 alizoshiriki kwenye klabu ya United.
Mkataba wake na Manchester United utamalika mwaka 2018.
Winga huyo alijiunga na timu ya Borussia Dortmund msimu uliopita kwa mkopo wa miezi minne, lakini alishiriki katika mechi 12 kabla ya kurudi katika timu yake ya Manchester United.

Post a Comment

 
Top