0
Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC imesema itazishitaki serikali za Uganda na Djibouti kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa kwa kushindwa kumtia nguvuni Rais wa Sudan Omar al Bashir alipozuru katika nchi zao.
Bashir anatuhumiwa kwa mauaji ya kimbari,uhalifu dhidi ya binaadam pamoja na kusababisha vita katika jimbo la Darfur.
Amekuwa akikana mashikata hayo.
Bashir alisafiri kwenda Uganda na Djibouti mwaka huu.
ICC inasema kuwa nchi hizo mbili zilipaswa kumtia nguvuni Bashir kwakuwa zilisaini mkataba na makahama hiyo.

Post a Comment

 
Top