0
-Watoto wa Kawe washiriki michezo na burudani mbalimbali

Katika kumalizia maadhimisho ya sikukuu ya Idd iliyoadhinishwa wiki hii, taasisi ya Vijana ya SuSo ya Kawe jijini Dar e salaam iliandaa tamasha la watoto lililofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers ambapo kampuni ya TBL Group ilikuwa mmoja wa wadhamini.

Katika tamasha hilo watoto kutoka eneo la Kawe na vitongoji mbalimbali walishiriki kucheza michezo mbalimbali ya watoto ,kucheza muziki na kufanya mashindano ya kuchora ,mashindano yam bio na kukimbia kwenye magunia.

Baadhi ya watoto walioshiriki tamasha la taasisi ya vijana ya SuSo

Baadhi ya watoto walioshiriki tamasha la taasisi ya vijana ya SuSo wakishindana mbio za magunia katika viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam.Tamasha hilo lilidhaminiwa na kampuni ya TBL Group.

watoto idd

Baadhi ya watoto walioshiriki tamasha la taasisi ya vijana ya SuSo wakishindana kukimbia katika viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam.Tamasha hilo lilidhaminiwa na kampuni ya TBL Group.

Vijana kutoka taasisi ya SuSo wakiangalia michezo ya watoto katika viwanja vya Tanganyika Packers

Vijana kutoka taasisi ya SuSo wakiangalia michezo ya watoto katika viwanja vya Tanganyika Packers.

Meneja Uhusiano wa TBL Group

Meneja Uhusiano wa TBL Group,Editha Mushi akiwafundisha kuchora baadhi ya watoto waliohudhuria tamasha la watoto lililoandaliwa na taasisi ya vijana ya SuSo na kufanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers-Kawe jijini Dar es Salaam.

Meneja Uhusiano wa TBL Group,Editha Mushi

Meneja Uhusiano wa TBL Group,Editha Mushi akisalimia baadhi ya watoto waliohudhuria tamasha la watoto lililoandaliwa na taasisi ya vijana ya SuSo na kufanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers-Kawe jijini Dar es Salaam.

Watoto walishiriki michezo ya aina mbalimbali na kugawiwa zawadi

Watoto walishiriki michezo ya aina mbalimbali na kugawiwa zawadi.

watoto eid 14

watoto eid 15

Post a Comment

 
Top