Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) ilikuwa imalizike Jumapili kwa michezo 10 kupigwa lakini katika mchezo wa Manchester United na Bournemouth uliokuwa ukitaraji kupigwa Old Trafford ulihairishwa kutokana na sababu za kiusalama.
Sababu ya kuhairishwa ni kuonekana kwa kitu ambacho kilidhaniwa kuwa ni bomu la mlipuko hivyo mchezo ukahairishwa ili kuzuia madhara ambayo yangeweza kujitokeza iwapo bomu hilo lingelipuka hivyo mchezo ukasimamishwa na mashabiki kutolewa uwanjani kwa usalama ili kuhakikisha hakuna madhara ambayo yatajitokeza.
Baada ya kufanyika uchunguzi kumeonekana kuwa halikuwa bomu kama ilivyodhaniwa hapo awali.
Kilichokutwa ni kifaa ambacho kinatumika kufanya mazoezi ili kuonyesha kama wanyama wanaotumika katika usalama wanauwezo wa kutambua kitu kilichokuwa ni mlipuko au sio mlipuko.
Inasemekana kuwa kifaa hicho kiliachwa na moja ya kampuni ambayo ilikuwwa ikifanya mazoezi karibu na eneo hilo hivyo wakati wakiondoka wakasahau kuchukua kifaa hicho ambacho baada ya watu wa usalama kukipata walikiharibu kwa tahadhari kama linaweza kutokea jambo lolote ambalo sio la kiusalama.
Aidha baada ya taarifa hiyo, tayari kumetolewa taarifa kuwa mchezo wa Manchester United na Bournemouth utachezwa siku ya Jumanne saa 4 usiku.
Post a Comment