0
Mkimbiaji wa mbio fupi Kariman Abuljadayel amekuwa mwanamke wa kwanza kutoka Saudi Arabia kushiriki katika mbio za 100m Olimpiki.
Abuljadayel, 22, aliyekuwa amevalia vazi la kujifunika mwili pamoja na hijab, hakufanikiwa kufuzu baada ya kumaliza nambari saba kundi la tatu la wanariadha wanane walioshindana hatua ya awali ya kufuzu.
Kariman AbuljadayelImage copyrightAFP
Muda wake ulikuwa sekunde 14.61.
Raia wa Afghanistan Kamia Yousufi pia alikimbia akiwa amevalia hijab na vazi la kujifunika vyema mwili, na ndiye aliyemaliza wa mwisho kundi hilo muda wake ukiwa sekunde 14.02.
Mwanariadha wa mbio za wastani Sarah Attar alikuwa mwanamke wa kwanza kuwakilisha Saudi Arabia kwenye mashindano ya mbio Olimpiki, aliposhiriki Michezo ya London 2012.
Saudi Arabia ilikuwa imewapiga marufuku wanawake kushiriki Olimpiki lakini marufuku hiyo ikaondolewa 2012.

Post a Comment

 
Top