0
BARAZA la Watoto nchini limeitaka jamii kuepuka matukio ya vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia katika kipindi hiki cha Sikukuu ya Idd el Fitr na maishani kwa ujumla.
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa taifa wa baraza hilo, Ameir Haji Khamis wakati akitoa tamko la baraza hilo kwa jamii katika kuadhimisha sikukuu ya Idd inayotokana na kumalizika kwa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Alisema katika kipindi cha sikukuu, hasa za Idd, matukio mengi ya vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo ubakaji vimekuwa vikijitokeza kwa wingi na kuiweka jamii hasa wazazi katika hali ya wasiwasi.
Alisema matukio hayo yamekuwa yakisababisha madhara makubwa kwa jamii ya wanawake na watoto huku mengine yakisababisha mimba kwa wanafunzi wa shule za msingi na kuwakosesha elimu.
“Baraza la watoto linaiomba jamii kusherehekea sikukuu ya Idd kwa amani na utulivu mkubwa kuepuka matukio ya uovu na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia na ubakaji,” alisema.

Post a Comment

 
Top