0
Uturuki imesimamisha kwa muda safari za nje kwa wasomi wote nchini humo, kama njia moja ya kuwaandama watu waliohusika katika jaribio la mapinduzi lililotibuka.
Zaidi ya watu 50,000 wamekamatwa, kufutwa au kusimamishwa kazi wakiwemo walimu wapatao 21,000.
Rais wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdogan kwa sasa anafanya kikao na maafisa usalama wa nchi na baraza lake la mawaziri.
Ni mara ya kwanza tangu arudi mjini Ankara kwake kufanya mkutano huo na wakuu serikali na vilevile wakuu wa kijeshi wanaomuunga mkono, tangu jaribio la kupindua serikali yake kufeli hapo Ijumaa iliyopita.

KUANDAMA WAASI UTURUKI

15,200
walimu na wahudumu wengine waliofutwa
1,577
wakuu wa vitivo waliotakiwa kujiuzulu
  • 8,777 wafanyakazi wa wizara ya mambo ya ndani waliofutwa
  • 1,500 wafanyakazi wa wizara ya fedha waliofutwa
  • 257 watu waliofutwa afisi ya waziri mkuu
Reuters
Rais Erdogan anajaribu kurudisha utulivu nchini humo lakini pia anashtumiwa kwamba anawalenga wapinzani wake akitumia kisingizio hicho cha jaribio la mapinduzi lililoshindwa.
Zaidi ya wasimamizi wa vitivo vya vyuo vikuu wapatao 1,577 wametakiwa kujiuzulu pamoja na walimu 21,000 na maafisa katika wizara ya elimu karibu 15,000.
Punde tu jaribio hilo la mapinduzi lilipotibuka, wengi wa wanajeshi, maafisa usalama na hata watumishi wa umma walikamatwa au kufutwa kazi.
Kulengwa kwa wizara ya elimu kunatokana na dhana ya utawala wa Uturuki kuwa mhubiri mashururi na mwenye utata Fethullah Gulen, aliyeko Marekani kwa sasa, alihusika na njama hiyo ya kupindua serikali.

Post a Comment

 
Top