0
Mkuu wa mafunzo na Utendaji Kivita wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Meja Jenerali Issa Nassoro amezitaka Timu teule za Jeshi kutobweteka na Ushindi wanaoupata katika mechi za majaribio wanazocheza.
Kauli hiyo imekuja Mwisho mwa wiki wakati  Timu ya Mpira wa Pete (Netball) Wanawake ya jeshi la Wananchi wa Tanzania kudhihirisha ubabe wake baada ya kuifunga Timu ya Mpira wa pete ya Wananume ya kikosi cha Valentia Zanzibar -KVZ kwa Magoli 36 kwa 24 katika mchezo uliofanyika Mwishoni mwa wiki Visiwani Zanzibar
Mchezo huo uliofanyika Katika katika uwanja wa Polisi Bwawani Ulikuwa kivutio kikubwa kutokana na kuhusisha jinsi mbili tofauti  kwa maana ya Wanaume na Wanawawake lakini pia ukiwa na wachezaji mahiri kutoka katika Timu zote mbili ambao wamekuwa na majina makubwa katika mchezo huo.
Meja Jenerali Nassoro aliyekuwa katika Ziara ya kutembelea kambi ya Timu teule za jeshi za mpira wa Miguu,Pete,Kikapu  na Mpira wa Mikono zilizoweka kambi katika Visiwa vya Unguja Mjini Zanzibar alisema ameridhishwa na kambi licha ya Jitihada zaidi kuongezwa ili kujihakikishia ushindi.
Alisema anamatumaini Makubwa historia ya kuweka kambi Zanzibar kutazibeba Timu za Jeshi kwani Timu mbalimbali zilizowahi kuweka kambi Zanzibar zilipata Mafanikio hivyo Jeshi na Taifa tunategemea hilo kama eneo zuri kwa kambi ili kujiandaa vizuri.
meja jenerali nassoro
Mkuu wa mafunzo na Utendaji Kivita Meja Jenerali Issa Nassoro akizungumza na Wanamichezo (hawapo pichani) katika Kambi ya Bavuai ikiwa ni maandalizi kuelekea Michuano ya Afrika mashariki kwa majeshi ya nchi za Afrika  Mashariki yatakayofanyika Kigali Rwanda Agosti mwaka Huu. (Picha na Selemani Semunyu).
Baadhi ya wachezaji wa Timu teule wa JWTZ
Baadhi ya wachezaji wa Timu teule wa JWTZ wakimsikiliza mkuu wa mafunzo na Utendaji kivita Meja Jenerali Issa Nassor aliyetembelea kambi ya Timu hizo Mjini Zanzibar zinazotarajiwa Kushiriki mashindano ya majeshi kwa nchi za Afrika mashariki Agosti mwaka huu Rwanda.(Picha na Selemani Semunyu)
 “Niliamua kwa Makusudi kupendekeza kambi kuwa Zanzibar nimekuwa Mchezaji na Mwanamichezo muda mrefu najua faida za kuweka kambi Zanzibar ukilinganisha na maeneo mengine kama Dar es Salaam” Alisema Meja  Jenerali Nassoro
Katika michezo ya majaribio za Timu hizo Teule za jeshi  Katika Mchezo wa mpira wa Kikapu Timu ya Jeshi wameifunga Timu ya Mbuyuni kwa Vikapu 104 kwa 58 na kuifanya Timu hiyo kuendeleza ubabe ikiwa ni mchezo baada ya michezo yake ya Awali kuzifunga Timu mabingwa wa Mchezo huo kwa Zanzibar.
Timu hizo zilizochezea kichapo katika Mpira wa  Kikapu  JWTZ iliifunga Stone Town kwa Vikapu 69 kwa 48 wakati mchezo uliochezwa kabla JWTZ waliifunga polisi kwa Vikapu 68 kwa 49 michezo iliyochezwa katika Viwanja Vya Maisara.
Katika hatua Nyingine Timu ya Soka ya JWTZ inakumbukumbu ya kuifunga Mafunzo kwa mabao Mawili kwa moja ikiwa ni mchezo wa marudiano huku mchezo wa Kwanza Timu ya Jeshi ikiwa imeibuka kwa Ushindi wa mabao Mawili kwa Moja, Katika mchezo Mwingine JWTZ wameifunga jeshi la Kujenga Uchumi JKU kwa Magoli Mawili kwa Moja.
Katika Mpira wa Mikono  JWTZ wameifunga Vijana Combine kwa Magoli 37 kwa 16 wakati katika Mchezo mwingine JWTZ waliifunga Zanzibar Warriors kwa Magoli 36 kwa 16.

Post a Comment

 
Top