0
Mamia ya wafuasi wa serikali ya Sudan kusini wameandamana mjini Juba kupinga pendekezo la viongozi wa Afrika kutuma kikosi cha ziada cha jeshi la kulinda amani.
AU ilifikia uamuzi huo baada ya kutokea mauaji ya zaidi ya watu 300 juma lililopita baada ya majeshi watiifu kwa makamu wa rais Riek Machar kukabiliana na vikosi vya kulinda rais Salva Kiir.
Rais wa nchi hiyo Salva Kiir amepinga kutumwa kwa mwanajeshi yeyote zaidi ya wale 12,000 wa umoja wa mataifa ambao tayari wako Sudan Kusini.
IGAD imependekeza wanajeshi hao wa ziada kuilipiga jeki jeshi la kulinda amani la UNMISS ambalo katika siku za hivi punde limelaumiwa kwa kushindwa kabisa kulinda maisha ya raia.
Kikosi hicho cha UNMISS kinalaumiwa na viongozi wa IGAD kwa kushindwa kuwalinda raia moja ya malengo kuu ya kuwepo kwao huko.
Image captionZaidi ya watu 300 waliuawa juma lililopita baada ya majeshi watiifu kwa makamu wa rais Riek Machar kukabiliana na vikosi vya kulinda rais Salva Kiir.
Viongozi wengine akiwemo rais wa Uganda Yoweri Museveni wamepinga pendekezo la kuwekewa vikwazo dhidi ya ununuzi wa silaha Sudan Kusini.
Mapendekezo hayo ni miongoni mwa mengine 6 ambayo yanatarajiwa kuratibiwa na umoja wa mataifa ya Ulaya AU inayoendelea mjini Kigali Rwanda.
Umoja wa mataifa unasema kuwa watu takriban elfu 40 walilazimika kuhama makwao kufuatia mapigano hayo.
Mkutano huo wa viongozi wa muungano wa Afrika ulimalizika jana nchini Rwanda.

Post a Comment

 
Top