0
Katika jitihada za kukihami kikosi chao kabla ya kutetea taji lao, Mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza Leicester City wamemsajili kiungo cha kati wa Ufaransa Nampalys Mendy.
Mchezaji huyo zamani akiichezea klabu ya Nice ametia sahihi mkataba wa miaka minne kufanya shughuli nchini Uingereza.
Hata hivyo, Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 hajawahi kuitwa katika kikosi cha taifa cha Ufaransa.
Hadi tulipochapisha habari hizi haikuwa imebainika mkataba huo ni wa kitita cha pesa ngapi.
Mendy alijiunga na Nice mwaka wa 2013 akitokea klabu ya Monaco alikoichezea katika mechi 110 za ligi ya daraja ya juu Ligue 1 katika misimu 3.
Mendy ni mchezaji wa tatu kujiunga na Leicester baada ya kipa Ron-Robert Zielerand na mlinzi Luis Hernandez.

Post a Comment

 
Top