0
Moja ya mataifa ambayo yamejitoa kuisaidia serikali ya Syria katika mapambano dhidi ya kikundi cha IS huwezi kuacha kuitaja Urusi pamoja na idadi ya wanajeshi wake wanaouliwa nchini Syria kuzidi kuongezeka.
Kumekuweo na taarifa ya helikopta ya kivita ya Urusi kulipuliwa na kikundi cha IS ambao baadae walithibitisha kuhusika na shambulio hilo, shambulio lilitokea mashariki kwa mji wa Palmyra na kusababisha vifo vya marubani wawili waliokuwepo katika ndege hiyo.
Marubani ambao walipoteza maisha katika shambulio hilo walifahamika kwa majina kuwa ni Riafagat Khabibulin na Yevgeny Dolgin na walikuwa katika helikopta ya Syria iliyokuwa na namba M-25.
Baada ya marubani hao kupoteza maisha inaelezwa kuwa karibu wanajeshi 12 wa Urusi waliopo Syria wameuliwa tangu walipofika nchini humo Septemba, 2015 kwa ajili ya kumsaidia rais wa Syria, Bashar al-Assad dhidi ya IS na makundi mengine ambayo yanapambana na serikali.
Taarifa kutoka Urusi zinaeleza kuwa kutokana na marubani hao kulipuliwa katika helikopta na wanakikundi wa IS, marubani hao wamechaguliwa kuwania tuzo za kitaifa za Urusi licha ya kuwa wamepoteza maisha na familia zao zitawawakilisha.

Post a Comment

 
Top