0
Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza, Theresa May ameshinda katika awamu ya kwanza ya kuwania uongozi wa chama cha Conservative kwa kupata kura nyingi.
Kiongozi huyo mpya atachukua hatamu za uongozi kutoka kwa Waziri Mkuu aliyeko madarakani David Cameron, ambaye ameachia ngazi baada ya nchi yake kupiga kura ya maoni ya kujiondoa uanachama wa Umoja wa Ulaya.
May amezungumzia matokeo na ushindi wake kuwa alikuwa ni yeye pekee anayeungwa mkono zaidi na chama chake cha Conservative.
Hapo awali May alikuwa akiipigia chapuo Uingereza kusalia katika jumuiya ya umoja wa Ulaya, huku mpinzani wake wa karibu Andrea Leadsom yeye alipigia kampeni Uingereza kujiondoa.
Upigaji kura wa awamu ya pili utafanyika siku ya Alhamisi.Wagombea watatu wanatarajiwa kuchuana na hii ni baada ya Liam Fox ambaye alijipatia kura chache wakati huu na kuondolewa na Stephen Crabb alijitoa mwenyewe .

Post a Comment

 
Top