0
Nchini Marekani ,FBI wanasema itakuwa si jambo la kupendeza kufungua mashtaka ya jinai dhidi ya Hillary Clinton kwa kutumia barua pepe binafasi kushughulikia taarifa za siri za kiserikali wakati alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani.
Mkurugenzi mkuu wa kitengo hicho , James Comey,amesema mgombea huyo kupitia chama Democrat alifanya uzembe ingawa hakuna dalili ya kufanya makosa kwa makusudi.Msemaji wa kampeni wa Hillary Clinton, amesema kwamba Hilary ametambua makosa yake na alidhani jambo hilo lilishamalizika.
Lakini mpinzani wake, mgombea kutoka chama cha Republican Donald Trump amesema kwamba Hilarry hakujali usalama wa nchi na kama asiposhtakiwa itaonyesha jinsi gani mfumo ulivyoharibika nchini humo.
WAKATI HUO HUO
Image copyrightREUTERS
Ikulu ya Marekani imesema kwamba rais Barack Obama hatazungumzia uchunguzi wa FBI.Msemaji wa Ikulu ya Marekani amesema kwamba Obama ameweka msimamo huo kwa kuchelea kuonekana anaingilia kati uchunguzi huo.
Lakini katika saa kadhaa za tamko hilo la FBI, Rais Obama alionekana katika kampeni za Hillary Clinton katika jimbo la Marekani kaskazini.
Obama amesema kwamba ana imani na Hillary na kudai kwamba zaidi ya Hilary hajaona mwanaume ama mwanamke anayefaa kugombea nafasi hiyo zaidi Hillary. Mwezi uliopita Obama binafsi alimtangaza kumuunga mkoano Bi Hillary kuwa mgombea urais wa Marekani.

Post a Comment

 
Top