0
ISImage copyrightAP
Image captionKundi la Islamic State limedai kuhusika
Wizara ya afya nchini Iraq inasema kuwa idadi ya watu ambao sasa wanajulikana kuuawa kwenye shambulizi la kujitolea mhanga siku ya Jumapili mjini Baghdad imeongezeka hadi watu 250.
Shambulizi hilo ambalo kundi la Islamic State lilidai kutekeleza, ndilo baya zaidi kuwai kutokea mjini Baghdad tangu Marekani iongoze uvamizi nchini Iraq mwaka 2003.
Ripoti ya Uingereza kuhusu uvamizi huo inatarajiwa kuchapishwa hii leo. Mwenyekiti wake anasema ana matumaini kuwa ripoti hiyo itahakikisha kuwa kuingilia kati kwa njia ya kijeshi kiwango kama hicho, hakuwezi kutokea siku za usoni bila ya kufanyika udadisi kwa njia ya uangalifu mkubwa.

2. Mfalme wa Saudia kukabili hatari ya mashambulio

Image copyrightAFP
Mfalme Salman wa Saudi Arabia ameahidi kuchukua hatua kufuatia misururu ya mashambulizi ya kujitolea mhanga.
Akiyataja makundi yenye itikadi kali, Salman alisema kuwa atawakabili vikali wale wanaojaribu kuvuruga akili za vijana wake. Alikuwa akiongea siku moja baada ya maafisa wanne wa usalama kuuawa na bomu karibu na eneo takatifu mjini Medina.
Pia kulikuwa na mashambulizi mengine mawili maeneo tofauti ya nchi hiyo. Inaaminika kuwa Islamic State ndio walihusika kwenye mashambulizi hayo ambayo yamelaaniwa na madhehebu ya Sunni na Shia.

3. Mwanabalozi aliyetekwa Nigeria aachiliwa huru

Naibu balozi wa Sierra Leone nchini Nigeria ambaye alitekwa nyara Ijumaa iliyopita ameachiliwa huru. Meja Jenerali alitekwa nyara katika mkoa ulio kaskazini wa Kaduna, akiwa na dereva wake raia wa Nigeria.
Taarifa kidogo imetolewa na maafisa kutoka nchi zote lakini anaripotiwa kuwa katika afya nzuri. Afisa kutoka nchini Sierra Leone anasema kuwa hakuna fidia ililipwa.
Visa vya utekaji nyara ni tatizo kusini mwa Nigeria lakini sasa vinasambaa kwenda kaskazini mwa nchi.

4. Amnesty yasema maelfu wameathirika kiakili Sudan Kusini

Shirika la Amnesty International linasema kuwa maelfu ya watu nchini Sudan Kusini wana matatizo ya akili yanayotokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe na wengi hawana matumaini ya kupata matibabu.
Amnesty inasema kuwa watu wamelazimishwa kula nyama ya binadamu wakati wa mzozo huo ambao ulianza mwishoni mwa mwaka 2013.
Inasema kuwa kuna uhaba mkubwa wa huduma za kiafya kote nchini humom huku mara nyingi watu walio na matatizo ya akili hufungiwa gerezani.

5. Obama ampigia kampeni Clinton

Image copyrightAP
Rais wa marekani Barack Obama ameonekana kwa mara ya kwanza kwenye kampeni ya mgombea urais wa Democtratic Hillary Clinton. Mapema shirika la ujasusi nchini marekani FBI liolisema kuwa hakuna mashtaka dhidi ya Bi Clinton kuhusu kutumia E-mail yake ya kibinafsi kutuma na kupokea ujumbe wa siri wakati akiwa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni. Hata hivyo mpinzani wake wa Republican amesema kuwa Bi Clinton kutofunguliwa mashtaka inaonyesha kuwa uchaguzi tayari umevurugwa

Post a Comment

 
Top