0
Kitengo cha umoja wa mataifa kinachoshughulika na haki za binaadamu kimeiambia BBC kwamba watu wapatao laki tisa ikiwa ni pamoja na wanaume kwa wavulana wamekamatwa na wanamgambo wa ki Shia wakati wa makabiliano ya kuwaondoa wanamgambo wa dola ya kiislamu IS nje ya mji wa Fallujah mwezi uliopita bado hawajulikani walipo.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Rupert Colville, anasema kwamba ripoti ya kutisha kuhusu hatma yao alipewa na watu wengine waliokamatwa nje ya Fallujah wakati huo ingawa kwa sasa wameachiliwa .
Image copyrightO
Rupet anasema kwamba mashuhuda wameshuhudia wanaume wanne wakiuawa kwa kukatwa vichwa na askari,na makumi kuuawa kwa kupigwa risasi .
Coville amesema kwamba wafungwa wamekuwa wakitendewa unyama kwa kupigwa na kwamba wako katika hali mbaya,na hali ya huduma za kijamii imezorota kwani chakula na maji ni haba.
Naye waziri mkuu wa Iraq ameagiza uchunguzi wa haraka ufanyike.

Post a Comment

 
Top