0
SERIKALI imesema imedhamiria kuboresha mahusiano kati ya mashirika ya dini na yasiyo ya Serikali kupitia sera ya ushirikiano wa umma na sekta binafsi katika huduma za afya ili kuzidi kufikia idadi kubwa ya wananchi kwa urahisi.
Hatua hiyo inatokana na kumalizika kwa mradi wa kutunza na kusambaza dawa, hasa za kufubaza virusi vya Ukimwi (ARVs) uliodumu kwa miaka 10 
uliokuwa unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Misaada la Marekani (USAID).
Akizungumza katika hafla ya kumalizika kwa mradi huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya alisema licha ya kumalizika kwa mradi huo, lakini serikali imejipanga vizuri kuhakikisha upatikanaji wa dawa unaendelea.
Alisema katika bajeti ya wizara hiyo ya mwaka wa fedha 2016/17 wameweka kipaumbele kwenye dawa na kuongeza kuwa chini ya mradi huo mafanikio mengi yamepatikana.

Post a Comment

 
Top