0
Raia nchini Uswisi wanashiriki katika shughuli za kwanza kabisa za kura ya maoni, zinazofanyika kote Nchini humo kuamua kuanzishwa kwa kipato cha msingi bila ya masharti.
Iwapo kura hiyo itapitishwa, serikali ya Uswisi itakuwa ikiwalipa raia wake ambao wanaishi nchini humo kihalali, kiasi cha dola 2,500 kila mwezi, hata ikiwa wameajiriwa au la.
Baadhi ya wachanganuzi wa kiuchumi wanasema kuwa mfumo huo, utawasaidia pakubwa na bado utaiwezesha serikali kusalia na fedha katika hazina yake ya taifa.
Wanauunga mkono wanasema kwamba, hatua hiyo itasaidia pakubwa kukabiliana na umaskini na kuwapa watu uwezo wa kuamua namna wanavyoishi na kufanya kazi.
Lakini wanaoupinga miongoni mwao vyama vyote vikuu nchini Uswizi, wanahoji kuwa fedha hizo zitawafanya watu kuzembea bila ya kufanya kazi.

Post a Comment

 
Top