Wapiga kura nchini Uingereza wataanza kupiga kura ya kusalia ndani ya muungano wa mataifa ya bara Ulaya au la saa tatu kamili saa za Afrika Mashariki.
Watakapofika katika vituo vya kupigia kura wataulizwa swali moja tu kwenye karatasi hizo za kupigia kura.
Je Uingereza isalie kwenye muungano wa ulaya au ijiondoe kwenye muungano wa ulaya?
Vituo vya kupigia kura hiyo ya maamuzi, vinafunguliwa muda mchache kuanzia sasa.
Zaidi ya watu milioni 46 watashiriki katika zoezi hilo, la upigaji kura ya ndio au la.
Mara ya mwisho kwa uingereza kuandaa kura ya maoni kuhusiana na uanachama wake ilikuwa miaka 40 iliyopita wakatyi huo ikijulikana kama European Economic Community.
Post a Comment