0
Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, amesema kuwa taifa lake linauwezo wa kushambulia maeneo ya Marekani, katika bahari ya Pacific.
Rais Kim Jong alisema hayo baada ya taifa lake kufanikiwa kutekeleza majaribio ya makombora yenye uwezo wa kusafiri mwendo wa kasi hadi masafa ya kadri.
Image copyrightREUTERS
Image captionbwana Kim Jong mwenyewe alisimamia na kushuhudia majaribio hayo ya silaha hatari ya masafa ya kadri
Runinga ya taifa mjini Pyongyang, imetangaza kuwa bwana Kim Jong mwenyewe alisimamia na kushuhudia majaribio hayo ya silaha hatari ya masafa ya kadri.
Image copyrightREUTERS
Image captionWanachama wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa wamekutana na kuelezea kutamaushwa kwao
Wataalamu wa kijeshi wa Marekani na Korea Kusini wanasema kwamba kombora moja lilishindwa kulipuka ilihali la pili ilifaulu kwenda zaidi ya mamia ya kilomita.
Korea Kaskazini imesifia pakubwa uwezo wake huo wa kuunda silaha za kitonoradi.
Image copyrightAFP
Image captionKorea Kaskazini imesifia pakubwa uwezo wake huo wa kuunda silaha za kitonoradi.
Wanachama wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa wamekutana na kuelezea kutamaushwa kwao na hatua hiyo ya Korea Kaskazini.

Post a Comment

 
Top