0
Watu 200 waliokimbia kutoka kwa maeneo yaliyovamiwa na wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram nchini Nigeria, wamefariki kutokana na baa la njaa na ukosefu wa maji.
Shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka- MSF, linasema kuwa vifo hivyo viltokea mwezi uliopita, katika kambi moja duni ya wakimbizi wa ndani kwa ndani, Kaskazini- Mashariki mwa nchi hiyo.
MSF linasema kuwa uhaba huo wa vyakula na maji unatishia maisha ya wakimbizi zaidi wa ndani kwa ndani katika kambi ya wakimbizi ya Bama Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Kambi hiyo yamkini inawakimbizi takriban elfu 20,000 hivi.
Image captionUmoja wa mataifa unakisia kuwa machafuko yaliyosababishwa na wanamgambo wa Boko Haram maeneo ya Kaskazini Mashariki mwa Nigeria yamesababisha watu milioni 2 kutoroka makwao.
MSF inasema kuwa mmoja kati ya watoto watano katika kambi hiyo wanaugua utapiamlo.
Umoja wa mataifa unakisia kuwa machafuko yaliyosababishwa na wanamgambo wa Boko Haram maeneo ya Kaskazini Mashariki mwa Nigeria yamesababisha watu milioni 2 kutoroka makwao.

Post a Comment

 
Top