0
Waziri mkuu nchini Uturuki Ahmet Davutoglu atajiuzulu katika kikao kisicho cha kawaida cha chama chake baadaye mwezi huu.
Ripoti zinasema kikao hicho kitafanyika tarehe 22 mwezi Mei baada ya Davutoglu kufanya mazungumzo na viongozi wa chama.
Uvumi kuhusu kujiuzulu kwake umekuwa ukiendelea tangu Davutoglu kukutana na rais Reccep Tayyip Erdogan siku ya Jumatano.
Anadaiwa kupinga wazo la Erdogan kuiweka nchi hiyo katika mfumo wa serikali ya rais mwenye mamlaka.
Image copyrightGetty
Image captionRais Reccep Teyyip Erdogan
Siku ya Alhamisi msaidizi wa rais, Cemil Ertem alionekana kuthibitisha ripoti aliposema kuwa hakutakuwa na uchaguzi wa ghafla kufuatia uchaguzi wa kiongozi mpya.
Pia aliiambia runinga ya Uturuki kwamba taifa hilo na uchumi utakuwa thabiti zaidi wakati ambapo waziri mkuu ambaye ni mwandani wa rais Erdogan atachukua mamlaka.
Bw Erdoga alimchagua Davutoglu kumrithi kama mkuu wa chama cha AK baada ya yeye kuchaguliwa rais 2014.

Post a Comment

 
Top