0
Meneja wa kilabu ya leicester Claudio Ranieri amewataka nyota wake katika kikosi chake kusalia katika timu hiyo kwa mwaka mmoja zaidi.
Mbweha hao waliwashangaza wengi kwa kushinda ligi hiyo baada ya kutumia pauni milioni 57 pekee msimu huu.
Winga Riyad Mahrez ,mshambuliaji Jamie Vardy na kiungo wa kati N'golo Kante ni miongoni mwa wachezaji wa klabu hiyo wanaotarajiwa kuondoka na kujiunga na timu nyengine msimu ujao.
''Nina matumaini tele'',alisema Ranieri.''Musiende''.
Image copyrightGetty
Image captionNyota wa Leicester
''Mukienda timu nyengine huenda musishirikishwe katika mechi''.
Wahandishi wa habari walimpatia heshima kwa kusimama kocha huyo wa Itali aliyechukua mahala pake Nigel Pearson msimu uliopita wakati alipowasili kwa mkutano na vyombo vya habari.

Post a Comment

 
Top