Msanii Snura Mushi ambaye wimbo wake wa Chura ulipigwa marufuku na serikali ya Tanzania ameomba radhi na kuahidi kutekeleza maagizo ya serikali.
Hata hivyo, bado ametetea video zilizotolewa za wimbo huo akisema zilitolewa tu kwa ajili ya YouTube.
Wimbo huo ulipigwa marufuku na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambayo ilisema "maudhui ya utengenezwaji wa video ya wimbo huo “haiendani na maadili ya Mtanzania.”
Mamlaka hiyo ilisema kazi hiyo inadhalilisha tasnia ya muziki.
Serikali ilipiga marufuku maonyesho yote ya hadhara ya Snura hadi pale atakapokamilisha usajili wa kazi zake za Sanaa katika Baraza la Sanaa la Taifa (Basata).
Akizungumza na wanahabari akiwa ameandamana na meneja wake, Snura amesema amechukua hatua na kusajiliwa rasmi kwa ajili ya shughuli za kisanii.
Post a Comment