WANACHAMA 29 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamevuliwa uanachama na wengine sita kushushwa vyeo mkoani Shinyanga, kutokana na kile kilichoelezwa ni kukisaliti wakati wa uchaguzi mkuu. Miongoni mwa waliovuliwa uongozi ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Wilaya ya Shinyanga Vijijini.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Katibu wa CCM wa
Pia aliwataja wengine na vyeo vyao kwenye mabano ni Charles Nkwabi (Katibu Kata ya Kisuke) kata ya Ngogwa, Wilfred Sazia (Mwenyekiti Kata Ngogwa), Samwel Gachu ambaye ni Katibu Mwenezi kata ya Isaka. Viongozi wengine waliovuliwa nyadhifa ni Peter Kigingi (Mwenyekiti Kata ya Bukomela) na Japhet Mabula ambaye ni Katibu Kata ya Mjini Kahama.Mkoa wa Shinyanga, Saad Kusilawe alisema uamuzi huo umetokana na kikao cha Halmashauri Kuu. Wengine waliovuliwa madaraka na vyeo vyao katika mabano ni Edward Lubinza (Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya) na Ng’honge Nkwabi (Kamanda wa UVCCM ) ambao wote ni wa Wilaya ya Shinyanga Vijijini.
Kusilawe alisema kwa mujibu wa Katiba ya CCM Toleo la mwaka 2012 Ibara ya 93, Kifungu kidogo cha 14 kinatoa mamlaka kwa Halmashauri Kuu ya Mkoa, kumchukulia hatua mwanachama yeyote atakayedhihirika kukosa sifa ya chama hicho.
Akizungumzia viongozi waliovuliwa uongozi na uanachama , alisema Kanuni ya Maadili Toleo la 2012 Ibara ya 8 inasema kosa kubwa kuliko yote ndani ya chama ni kusaliti na kukiweka chama katika hali ya kushindwa katika uchaguzi na mtu anayefanya kosa hilo, lazima afukuzwe Kwa upande wa Katiba ya CCM, alisema watu hao wamevunja Katiba Ibara ya 5 inayosema malengo ya chama hicho ni kushinda uchaguzi wa Serikali Kuu na wa Serikali za Mitaa Bara na Visiwani, hivyo mwanachama yeyote atakayekwenda kinyume na malengo hayo, atakuwa amekosa sifa ya kuwa mwanachama.
Wakati huo huo, alisema wanachama 12 walijivua wenyewe, hivyo Kamati Kuu ilibariki kuondoka kwao.
Post a Comment