0
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) anayeshughulikia Utumishi na Utawala Bora, Selemani Jafo

BAADA ya serikali kuwapa uraia wananchi wa Kambi ya Katumba, wilayani Nsimbo mkoani Katavi, wananchi hao wanatarajiwa kufanya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu ambao maandalizi yake yameanza.
Kwa mujibu wa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jaffo, katika kata ya Katumba, vijiji ambavyo havikufanya uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2014 ni 14 na vitongoji ni 51.
Jaffo alisema uchaguzi huo ulishindwa kufanyika kwa sababu kata hiyo ilikuwa na kambi ya wakimbizi ambao walikuwa hawajapata uraia wa Tanzania kwa mujibu wa sheria za nchi.
“Baada ya serikali kuwapa uraia wananchi wa maeneo hayo, Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo inaendelea na maandalizi ya kufanya uchaguzi mdogo katika vijiji na vitongoji hivyo,” alisema.
Alisema tayari katika bajeti ijayo ya mwaka 2026/17 zimetengwa Sh 3,300,000 ili kuwezesha zoezi hilo kufanyika. Naibu Waziri alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Nsimbo, Richard Mbogo (CCM).
Katika swali lake, Mbogo alisema chaguzi za madiwani zilifanyika katika Kambi ya Wakimbizi Katumba mwaka 2015, alihoji ni lini serikali itapeleka fedha ili kukamilisha chaguzi za serikali za vijiji na mitaa katika Kambi ya wakimbizi Katumba.

Post a Comment

 
Top