0

Serikali ya Uganda imepiga marufuku matangazo ya moja kwa moja yanayopinga uchaguzi wa rais Yoweri Museveni.
Usalama katika mji mkuu umeimarishwa kabla ya maandamano yalioitishwa na chama cha Forum for Democratic Change .
Wiki iliopita agizo la mahakama lilipiga marufuku kampeni za chama hicho.
Mahakama ya juu nchini Uganda iliunga mkono uchaguzi wa Museveni licha ya kupingwa.
Image captionWafuasi wa Besigye
Vyombo vya habari nchini Uganda vimetakiwa kutofanya matangazo ya moja kwa moja na wanachama wa upinzani ambapo wanapinga kuchaguliwa kwa rais Museveni.
Matangazo ya moja kwa moja runingani yamekuwa jambo muhimu katika habari wakati wa uchaguzi uliopita.
Wiki iliopita agizo la mda lililotolewa na mahakama liliwazuia wanaoandamana na waliokongamana kama vile kwenye ibada wakiongozwa na kiongozi wa upinzani Kizza Besigye.
Hatahivyo agizo hilo limekosolewa kwa kuwa hakukuwepo kwa makundi ya upinzani wakati wa kikao hicho cha mahakama.
Image captionMuseveni
Besigye ambaye alikuwa wa pili katika uchaguzi alipinga matokeo ya kura hiyo akisisitiza kuwa alishinda.
Wafuasi wake walitarajiwa kwenda kinyume na amri hiyo ya mahakama na kufanya maandamano siku ya Alhamisi.
Kuna wanajeshi wengi pamoja na maafisa wa polisi mji Kampala.
Nyumba ya Besigye imefungwa na haruhusiwi kutoka nje.
Rais Museveni anatarajiwa kuapishwa wiki ijayo Alhamisi

Post a Comment

 
Top