0
Wabunge nchini Kenya wanatarajiwa kupiga kura, kwa mara nyingine, ya kupitisha ama kupinga mswada wa sheria kuhusu usawa wa jinsia katika nyadhifa za uteuzi na siasa.
Kwa mujibu wa Katiba ya Kenya, nyadhifa zote za uteuzi na uchaguzi katika afisi za umma hazifai kuchukuliwa na zaidi ya theluthi mbili ya jinsia moja, iwe wanawake ama wanaume.
Mswada huo ulihitaji wabunge kuungwa mkono na wabunge 233 ndipo uidhinishwe lakini idadi ya wabunge waliohudhuria kikao, yenyewe haikufikia kiwango hicho.
Baada ya kura kupigwa, wabunge 179 waliunga mkono mswada huo, 16 wakapinga na 5 wakakosa kutangaza msimamo wao.
Wiki iliyopita mswada huo ulifeli ambapo ni wabunge 195 pekee waliouunga mkono, 28 wakaupinga, wawili wakakosa kutangaza msimamo wao huku 24 wakikataa kupiga kura.
Mwenyekiti wa muungano wa wabunge wanawake nchini Kenya Cecily Mbarire alikuwa awali ameeleza matumaini kwamba mswada huo ungeidhinishwa lakini hilo halikuwa.
"Tuna matumaini kuwa mswada huu utaptishwa hivi leo, tumekuwa tukizungumza na wenzetu wanaume, na kuwarai kutuunga mkono, na tuna matumaini,” alisema awali.
Kura ya leo ilipigwa siku ya mwisho kabla ya wabunge kwenda likizoni, na kwa kawaida kikao kama hicho huhudhuriwa na wabunge wachache.
Wabunge wanatarajiwa kwenda likizo ya mwezi mmoja baada ya kikao cha leo alasiri.
Rais Uhuru Kenyatta, ambaye ni kiongozi wa muungano wa Jubilee, ulio na wanachama wengi bungeni, alikuwa amewaomba wabunge kupitisha mswada huo.
OdingaImage copyrightAFP
Image captionBw Odinga amesema atahudhuria kikao cha leo cha Bunge
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga pia alitoa ombi sawa na hilo kwa wabunge wa muungano wake wa CORD.
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2013, wanawake hawakuchaguliwa katika nyadhifa za ugavana na useneta.
Kati ya wabunge 290 waliochaguliwa na wananchi mwaka 2013, asilimia 5.5 pekee ya wanawake ndio waliochaguliwa.
Kati ya wawakilishi wa wodi 1450, ni wanawake 88 pekee waliochaguliwa.
Bunge la kenya linajumuisha wabunge 290 waliochaguliwa na wananchi, wabunge 47 wanawake waliochaguliwa na wananchi kuwakilisha kaunti 47

Post a Comment

 
Top