Polisi nchini Ufaransa wametumia vitoa machozi kuwatawanya wafanyikazi wanaondamana na kufunga kiwanda cha kusafisha mafuta katika mji wa Marseille.
Polisi wanasema kuwa walikabiliana na upinzani mkali kutoka kwa waandamanaji ambao waliwarushia maguruneti na kuwasha moto barabarani.
Maandamano hayo ni sehemu ya misururu ya maandamano ya kupinga sheria mpya za kazi.
Vyama vya wafanyikazi vinasema kuwa mishahara katika viwanda vya mafuta itapungua kwa takriban asilimia 50, kutoka na mzozo na mgomo wa madereva wa malori na vitua vingi vya mafuta kote Ufaransa sasa vinaishiwa na mafuta.
Post a Comment