0
Rais wa Marekani Barack Obama ameelezea mikakati yake ya kubuni uhusiano thabiti na wa kudumu na Vietnam, siku moja tu baada ya kuliondolea taifa hilo la zamani la kikomunisti vikwazo vya silaha.
Mataifa hayo mawili yamekuwa yakihasimiana kwa muda mrefu tangu kumalizika kwa vita baridi na uvamizi wa Marekani miaka ya sabini.
Katika hotuba aliyoitoa katika mji mkuu Hanoi, Bwana Obama alisema kuwa kuboresha uhusiano wa kidiplomasia , miongo minne baada ya vita vya Vietnam, ni mfano bora wa uwiano.

Post a Comment

 
Top