0
Rais wa Marekani Barack Obama amewasili nchini Vietnam wakati anaanza ziara ya wiki moja barani Asia.
Maafisa nchini Marekani wanasema kuwa ziara hiyo ina lengo la kuboresha ushirikiano wa ulinzia na kiuchumi kati ya mataifa hayo ambayo ni mahasimu wa zamani.
Waandishi wa habari wanasema kuwa Marekani inataka kuiunga mkono Vietman na mataifa ya kusini mashariki mwa Asia yaliyo kwenye mzozo wa kikanda na China.
Vietnam inaripotiwa kutaka iondolewe vikwazo vya silaha ilivyowekewa na Marekani.

Post a Comment

 
Top