0
Kundi moja la balozi za bara Afrika mjini Delhi limeitaka India kuahirisha sherehe moja ya kitamaduni kufuatia kuuawa kwa mwanafunzi mmoja kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wiki iliopita.
Masunda Kitada Oliver alipigwa hadi kufariki na kundi moja la wanaume wa Kihindi Ijumaa iliopita baada ya majibizano mjini Delhi.
Watu wawili wamekamatwa kufuatia kisa hicho.
Balozi hizo zimesema kuwa hazitaki kushiriki katika kuadhimisha siku ya Afrika siku ya Alhamisi kufuatia misururu ya mashambulizi dhidi ya wanafunzi kutoka Afrika.
''Hii ni kwa sababu jamii ya Kiafrika nchini india ,wakiwemo wanafunzi wanaendelea kuomboleza kuwaenzi wanafunzi wa Afrika waliouawa akiwemo bwana Oliver,alisema Alem Tsehage Woldremariam'',kiongozi wa mabalozi wa Afrika nchini India.
Mnamo mwezi Februari,mwanafunzi mmoja wa Tanzania alipigwa na kuvuliwa nguo na kundi moja katika mji wa Kusini wa Bangalore.

Post a Comment

 
Top